Maafisa wa Hawaii wazuia watalii kwenda kisiwa cha Maui
14 Agosti 2023Matangazo
Mji wa kihistoria wa Maui umeharibiwa vibaya na moto mkubwa kabisa wa nyikani kuwahi kushuhudiwa ambao pia umesababisha vifo vya zaidi ya watu 90.Karibu wakaazi 46,000 pamoja na wageni wamekimbilia katika uwanja wa ndege wa Kahului ulioko Maui Magharibi, tangu kuibuka kwa janga hilo, hii ikiwa ni kulingana na Mamlaka ya Utalii ya Hawaii.Jana, wakazi wa Hawaii walifanya ibada maalumu kwa ajili ya wahanga wa moto huo, wakati wakijiandaa kuanzisha upya maisha. Gavana Josh Green amesema vyumba 500 vya hoteli vitatengwa kwa ajili ya wakazi wasio na makazi na vingine 500 kwa ajili ya wafanyakazi wa mamlaka ya masuala ya dharura ya shirikisho.