1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wa Afya wahofia mlipuko wa homa ya nyani Afrika

2 Agosti 2024

Maafisa wa afya barani Afrika wameelezea wasiwasi wao kuhusu kuongezeka kwa maambukizi ya homa ya nyani na kuonya juu ya hatari ya kuenea zaidi kwa ugonjwa huo kutokana na ukosefu wa matibabu na uhaba chanjo.

https://p.dw.com/p/4j20L
Kipimo cha  Corona huko Soweto Afrika Kusini.
Thabisle Khlatshwayo wakati wa majaribio ya chanjo ya COVID-19 nje ya Johannesburg, Afrika Kusini, Novemba 30, 2020.Picha: Jerome Delay/AP Photo/picture alliance

Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Afrika vimesema kwamba mwaka huu pekee, maambukizi ya homa ya nyani yameongezeka kwa asilimia 160 na kwamba ugonjwa huo tayari umeripotiwa katika nchi 10 za Afrika mwaka huu ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Kenya na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Milipuko ya ugonjwa wa homa ya nyani unaofahamika pia kama (Mpox) katika nchi za Magharibi imekuwa mara kadhaa ikidhibitiwa kutokana na matumizi ya chanjo na matibabu, lakini chanjo hizo hazipatikani katika nchi za Afrika.