1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaIran

Maafisa 11 wa polisi ya Iran wauwawa kwenye shambulizi

15 Desemba 2023

Maafisa 11 wa polisi wa Iran wameuawa katika shambulio linalodaiwa kufanywa na wapiganaji wa itikadi kali kwenye kituo cha polisi jimbo la kusini mashariki la Sistan-Baluchistan.

https://p.dw.com/p/4aBil
Iran | Polisi wa Iran
Sare ya polisi wa IranPicha: Icana News Agency/ZUMA/picture alliance

Naibu gavana wa jimbo hilo, Alireza Marhamati, ameliita shambulio hilo la kigaidi kwenye makao makuu ya polisi katika mji wa Rask na kwamba limegharimu maisha ya maafisa 11 wa polisi na kuwajeruhi wengine.

Televisheni ya taifa imeripoti kuwa baadhi ya washambuliaji pia wameuawa katika ufyatulianaji ya risasi na vikosi vya usalama.

Shambulio hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo, ni moja kati ya mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea katika eneo hilo karibu na mpaka wa Afghanistan na Pakistan.

Hali ya ukosefu wa usalama imeshuhudiwa mara kwa mara katika jimbo la Sistan-Baluchistan, ambalo pia linapakana na Afghanistan - na kuhusisha pia magenge ya ulanguzi wa dawa za kulevya, uasi kutoka jamii ya wachache ya Baluchi na waumini wenye misimamo mikali ya dini.