1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walinzi sita wa mpakani wa Iran wauwawa

21 Mei 2023

Katika tukio lililotokea leo hii walinzi sita wa mpaka wa Iran waliuawa wakati wa makabiliano na kundi lenye kujihami kwa silaha katika mkoa wa Sistan-Baluchistan, kusini mashariki mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4Rd5j
Iran Soldaten
Picha: Iranian Army/AA/picture alliance

Tovuti inayomilikiwa na mahakama ya Mizan imemnukuu mwendesha mashtaka wa eneo hilo Mehdi Shamsabadi akisema walinzi hao waliuawa huko Saravan, karibu na mpaka wa Iran na Pakistan.Eneo la Sistan-Baluchistan linalokabiliwa na umaskini, ambalo pia inapakana na Afghanistan, ni kitovu cha  mapambano cha magenge ya biashara ya magendo ya dawa za kulevya pamoja na waasi kutoka makundi ya wachache ya Baluchi na Waislamu wenye itikadi kali kutoka katika madhehebu ya Sunni.Itakumbukwa Machi 11, shirika la habari la serikali IRNA liliripoti tukio la polisi wawili kuuwawa kwa kupigwa risasi wakati wa mapigano na kile kilichosemwa "wahalifu" katika mkoa huohuo.