Lula da Silva aikosowa Ulaya kwa kutobadilika
8 Desemba 2023Serikali ya Lula da Silva ilitumaini kufikiwa kwa makubaliano kwenye mkutano wa kilele baina ya Ulaya na Amerika Kusini, baada ya majadiliano ya zaidi ya miaka 20, ambayo ndani yake kunatarajiwa kuanzishwa ukanda mkubwa zaidi huru wa kibiashara ulimwenguni.
Umoja wa Ulaya unaitaka Amerika ya Kusini kuhakikishiwa ikiwa uzalishaji wa bidhaa za kilimo zitakazouzwa nje hautaharibu msitu wa mvua wa Amazon au mifumo mingine muhimu ya ikolojia.
Soma zaidi: Viongozi duniani walaani uvamizi wa majengo ya utawala Brazil
Hata hivyo, Rais Lula da Silva anasema Ulaya haitaki kubadilika na kukosoa vikali sera ya "kujilinda" ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, aliyeyapinga makubaliano hayo walipokutana pembezoni mwa mkutano wa mazingira wa COP28 huko Dubai.