1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lukashenko adokeza kupelekwa silaha za nyuklia kutoka Urusi

26 Mei 2023

Rais wa Balarus Alexander Lukashenko amedokeza kwamba silaha za nyuklia zinazotoka Urusi tayari zinapelekwa nchini humo, baada ya mataifa hayo mawili kusaini makubaliano ya kupelekwa kwa silaha hizo.

https://p.dw.com/p/4RryR
Belarus Präsident Lukaschenko bei Truppenbesuch
Picha: Belarus' Presidential Press Office/AP/picture alliance

Ingawa Lukashenko hakubainisha zitakapowekwa silaha hizo, taarifa za awali zinasema zitapelekwa karibu ya mpaka na Poland.

Rais wa Urusi Vladimir Putin mapema mwaka huu alitangaza kupelekwa kwa makombora ya masafa mafupi nchini Belarus, katika hatua inayochukuliwa kama onyo kwa mataifa ya Magharibi yanayoongeza usaidizi wa kijeshi nchini Ukraine.

Mpinzani wa Lukashenko, Sviatlana Tsikhanouskaya amelaani hatua hiyo na kuyaomba mataifa washirika kuchukua hatua za kuizuia.