Lori ya mafuta yalipuka Uganda na kuwauwa watu 11
23 Oktoba 2024Matangazo
Polisi wamesema ajali hiyo ilitokea mida ya saa tisa alasiri hapo jana katika mji wa Kigogwa, takriban kilometa 25 kaskazini mwa mji mkuu Kampala. Taarifa ya Polisi imeongeza kuwa baadhi ya miili iliharibiwa na moto kiasi cha kutotambulika huku majengo manne yakiteketezwa pia na moto huo. Lori hiyo ililikuwa ikisafiri kutoka Kampala kwenda Gulu kaskazini mwa Uganda, ambayo ni safari ya takriban kilomita 650. Katika miaka ya hivi karibuni, Uganda imeshuhudia matukio kadhaa kama hayo ambapo watu hukimbilia kuchota mafuta kutoka kwa lori zilizopata ajali. Haya yanajiri wakati mnamo Oktoba 15, lori la mafuta liliripuka kaskazini mwa Nigeria na kuua zaidi ya watu 170.