1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya yaanza tena kuchimba mafuta

22 Januari 2024

Serikali ya Libya imeanza tena uzalishaji wa mafuta katika kisima cha Al-Sharara, kinachozalisha robo ya mafuta yanayosambazwa kote nchini humo, wiki mbili baada ya maandamano yaliyosababisha kufungwa kwa kisima hicho.

https://p.dw.com/p/4bXF0
Kinu cha mafuta Libya.
Kinu cha mafuta Libya.Picha: Petros Karadjias/AP/picture alliance

Shirika la Mafuta la Taifa (NOC) lilitangaza kuondolewa kwa zuio hilo na kurejeshwa kwa uzalishaji kamili kwenye kisima cha Al-Sharara ambacho kwa kawaida huzalisha hadi mapipa 315,000 kwa siku.

Kundi la waandamanaji la Fezzan Gathering lililojikita mkoa wa Oubari lilitangaza siku ya Jumapili (Januari 21) kwamba walifikia makubaliano na NOC ya kumaliza mkwamo huo na baadaye kuchapisha taarifa ya makubaliano hayo kwenye ukurasa wa Facebook.

Kulingana na kundi hilo, wamehakikishiwa na mbabe wa kivita nchini humo, Khalifa Haftar, anayeunga mkono moja ya serikali zinazohasimiana za Libya.