1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leicester City yarejea kwenye ligi ya Premier

27 Aprili 2024

Klabu ya Leicester City imerejea kwenye Ligi ya Premierjana Ijumaa baada ya wapinzani wake Leeds United kucharazwa mabao 4-0.

https://p.dw.com/p/4fFC5
Soka | Premier League | Robert Huth akiwa na kombe
Leicester City ilichukua ubingwa wa PL mwaka 2016 lakini ilishushwa daraja msimu uliopita na sasa inarejea kwenye ligi hiyoPicha: David Klein/Sportimage/PA/picture alliance

Matokeo hayo yanaifanya klabu hiyo ya Leicester Citykuongoza daraja la pili kwa pointi 94 ikiwa imebakiwa na michezo miwili, ikifuatiwa na Leeds yenye pointi 90 na mechi moja mkononi.

Ipswich Town inayoshika nafasi ya tatu na pointi 89, ikiwa bado na michezo mitatu huenda ikaiondoa Leeds kwenye nafasi ya pili ikiwa itaifunga Hull watakapokutana hii leo. Na ikiwa watashinda mechi zote watapanda daraja, huku Leeds wakilazimika kucheza mechi ya kufuzu.

Leicester ilichukua ubingwa wa PL mwaka 2016 na kuushtua ulimwengu wa soko, lakini walishushwa daraja sambamba na Leeds na Suothampton kwenye msimu uliopita, lakini kikosi hicho kimekuwa kikipambana kurejea na hasa baada ya kuiacha nyuma Leeds iliyokuwa ikishika nafasi ya pili kwa pointi 12.

Siku ya Jumanne watakabiliana na Southampton ambayo pia inatupia jicho ligi kuu baada ya kufungwa michezo sita kati ya 11 huko nyuma.