1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Kyiv yaiomba Ujerumani kuipa makombora ya Taurus

27 Mei 2023

Ukraine imeomba Ujerumani kuipatia makombora aina ya Taurus, ili kuikabili Urusi hii ikiwa ni kulingana na wizara ya ulinzi ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4RtSF
Kombora aina ya Taurus kama linavyoonekana katika picha iliyopigwa Septemba 25 katika maonyesho ya siku ya majeshi ya korea Kusini.
Ukraine imekuwa ikiyaomba mataifa ya magharibi kuendelea kuisaidia kwa silaha, ingawa mataifa hayo yanahofia kuipatia makombora ya masafa marefu.Picha: Jung Yeon-Je/AFP/Getty Images

Msemaji wa wizara hiyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, Ukraine imewafikishia ombi hilo hivi karibuni.

Makombora hayo yana uwezo wa kwenda umbali wa kilomita 500, na hiyo itaiwezesha Ukraine kulishambulia eneo la Urusi.

Washirika wa Kyiv hadi sasa wamekuwa na mashaka ya kuipatia silaha zinazoweza kufika Urusi.

Soma Zaidi: Ukraine yadungua droni 36 katika mashambulizi ya usiku

Siku ya Ijumaa, kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amerudia tena matamshi yake kwamba taifa hilo litaipa silaha Ukraine ambazo hazitatumika kuishambulia ardhi ya Urusi.