Bei ya mafuta imepanda kote ulimwenguni hali ambayo imesababisha bei za bidhaa nyingine muhimu kupanda na kuongeza gharama za maisha. Bei ya mafuta imeongezeka hadi kufikia zaidi ya dola 80 kwa pipa huku bei za gesi asili na makaa ya mawe zikifikia viwango vipya na kuvunja rekodi katika wiki chache zilizopita. Josephat Charo anajadili suala hili katika kipindi cha Maoni mbele ya Meza ya Duara.