Kundi la waasi la CODECO laua watu 14 mashariki mwa DRC
30 Agosti 2023Matangazo
Kiongozi wa shirika moja la kiraia Issa Atsidri amealiambia shirika la habari la AFP kuwa, wapiganaji wa CODECO waliwasili katika eneo la uchimbaji madini la Shaba na kuwaua watu 14.
Ameongeza kuwa, watu 10 wamejeruhiwa na wengine hawajulikani waliko.
Mwanachama mwandamizi wa kundi la vijana katika eneo hilo Jacques Uguzi Amopi ameeleza kuwa, miili 15 ikiwemo ya wanawake watatu ilipatikana na kuchukuliwa na jamaa zao.
Sababu ya shambulio hilo bado haijajulikana.
Waasi wa ushirika wa maendeleo ya Kongo CODECO ni moja kati ya makundi yenye silaha yanayoendesha oparesheni zao eneo la mashariki mwa DRC na lilizuka katika miaka ya 1990 na 2000 kufutia vita vya kikanda.