1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Hamas yatoa vidio ya mateka watatu wakiomba usaidizi

19 Desemba 2023

Kundi la wanamgambo la Hamas limetoa vidio ya mateka watatu wazee wanaodai kuwa Israel "imewatelekeza" na kuomba waachiliwe huru mara moja.

https://p.dw.com/p/4aJzq
Israel | Makubaliano ya kubadilishana wafungwa na mateka kati ya Israel na Hamas
Mmoja wa mateka Emily Hand waliochukuliwa na kundi la Hamas akimkubatia babake baada ya kuachiliwa huruPicha: Israel Defense Forces/REUTERS

Wazee hao wametambuliwa kuwa wakaazi wa kijiji cha Nir Oz kilichoko karibu na mpaka wa Israel na Gaza, na ambao walichukuliwa mateka na kundi la Hamas mnamo Oktoba 7.

Wake wa watatu hao ambao pia walikuwa wamechukuliwa mateka wameachiliwa.

Akizungumza kwenye vidio hiyo, mmoja wa wazee hao ameeleza kuwa wote wanaugua magonjwa sugu na wametoa wito wa usaidizi.

Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari amesema vidio hiyo inaonyesha "ukatili wa Hamas dhidi ya wazee wasiokuwa na hatia na ambao wanahitaji matibabu."

Mnamo mwishoni mwa mwezi uliopita, Israel na Hamas walibadilishana wafungwa na mateka, huku raia 100 wa Israel waliokuwa wameshikiliwa mateka wakiachiliwa huru wakati wafungwa 240 wa Palestina waliokuwa wamezuiliwa na Israel wakiachiliwa.

Wengi walioachiliwa huru na pande zote wakati huo walikuwa wanawake na watoto.