1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Hamas: Hatutoshiriki upatanishi hadi hujuma zisitishwe Gaza

17 Desemba 2023

Kundi la Hamas linalotawala Ukanda wa Gaza limesema halitashiriki mazungumzo yoyote ya kubadilishana wafungwa hadi pale Israel itakapositisha hujuma zote dhidi ya Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4aGkF
Mji wa Khan Yunis
Mashambulizi ya Israel - kujibu mauaji ya Hamas ya Oktoba 7- yamekuwa yakisababisha vifo vya watu kila siku Ukanda wa GazaPicha: MAHMUD HAMS/AFP/Getty Images

Hayo yameelezwa kupitia taarifa ya kundi hilo iliyotolewa leo Jumapili iliyoarifu pia kwamba pande zote zinazoongoza juhudi za upatanishi zimefahamishwa kuhusu msimamo huo.

Tangazo hilo limetolewa wakati maafisa wa Qatar - taifa ililojitwika dhima ya kuwa mpatanishi wa mzozo kati ya Israel na Hamas-  wamesema wanafanya mashauriano na pande zote hasimu ili kufanikisha mkataba mpya wa kusitisha mapigano.

Inaarifiwa kwamba maafisa wa Israel na Qatari walikutana hivi karibuni nchini Norway kujadili kuachiwa huru kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas kwa mabadilishano na wafungwa wa Kipalestina walio katika jela za Israel.

Wakati hayo yakijiri Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO limetahadharisha leo kuwa hali inazidi kuwa mbaya ndani ya Ukanda wa Gaza kutokana na mapigano yanayoendelea.

Shirika hilo limesema upatikanaji wa huduma za matibabu unasuasua hasa baada ya uharibifu uliofanywa kwenye hospitali kubwa ya Al-Shifa