Kumbukumbu ya miaka 25 ya shambulio la chuki dhidi ya wageni
30 Mei 2018Mhariri wa gazeti la Hannoversche Allgemeine Zeitung akizungumzia kuhusu kumbukumbu ya shambulio la kuchomwa moto nyumba ya Bibi Mevluede Genc raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki mjini Solingen anaandika:
"Mwaka 1993 bibi Mevluede Genc mwenye asili ya Uturuki alipoteza watoto wake wawili wa kike , wajukuu wawili na mpwa wake kutokana na shambulio la kuchomwa moto nyumba yake. Mtu anaweza kuelewa iwapo mtu kama huyu anaweza kuishi maisha yake yote akiwa na chuki. Mevluede Genc lakini alibakia muwazi kwa pande zote na kuendelea kuwa mjenzi wa daraja la maelewano. Kila mmoja iwe katika sehemu ya mauzo ama katika ofisi ya serikali tunapaswa kutafakari na kumwangalia bibi Mevluede Genc kama mfano. Bibi huyu kizee ambae hana majivuno, mpole ametufunza unyenyekevu na maridhiano."
Mhariri wa gazeti la Leipziger Volkszeitung kuhusiana na tukio hilo la kumbukumbu mjini Solingen anaandika kwamba historia ya maisha ya bibi huyu inamuacha mtu mdomo wazi. Mhariri anaendelea:
"Jana katika kumbukumbu ya miaka 25 bibi huyu mwenye umri wa miaka 75, baada ya kuuwawaa kwa watoto wake, bado anazungumzoa kuhusu maridhiano na kusameheana. Hili si jambo rahisi sana."
Gazeti la Neue Osnabrücker Zeitung linaandika kuhusu kashfa inayoikumba idara ya uhamiaji ya mjini Bremen kwa kuidhinisha maombi kiholela ya wahamiaji wanaoomba hifadhi. Mhariri anaandika.
"Tukiangalia shutuma za baraza la wafanyakazi dhidi ya idara ya uhamiaji na wakimbizi ya Ujerumani, utaona kwamba makosa ya ofisi hiyo ya uhamiaji mjini Bremen ni tone tu katika bahari. Baada ya hapo utaona kwamba viwango vya utendaji kupitia miongozo ya kulazimishwa , maombi hayo ya wakimbizi yalifanyiwa kazi kwa juu juu tu, bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina. Kwa mujibu wa hatua za haraka ili kutimiza sheria za kikatiba. Pamoja na hayo anapitisha mtu huyo aliyeamua ambaye ni mfanyakazi anayeifanya kazi hiyo bila ya kuwa na ujuzi unaohitajika."
"Mkuu wa zamani wa idara hiyo Frank-Juergen Weise aliomba ofisi ya kansela kuweka mfumo wa kuchunguza utaratibu kazi hizo, baada ya kauli mbiu maarufu ya kansela ya , tutaweza. Ni maeneo mangapi yameathirika, maelfu ama maelfu kadhaa."
Kuhusiana na mzozo wa kuunda serikali nchini Italia , gazeti la Mittelbayerische Zeitung la mjini Regensburg linaandika.
"Tofauti na jinsi Umoja wa Ulaya unavyofanya mahusiano yake na sera za kizalendo za siasa kali za mrengo wa kulia za rais wa Marekani Donald Trump , hatima hiyo inaikumba nchi jirani yetu ya Italia moja kwa moja. Mzizi wa fitina hapa ni wasi wasi wa kujitoa kwa Italia nchi yenye uchumi wa tatu mkubwa barani Ulaya kutoka katika sarafu ya euro ama masoko ya hisa yanavyoliangalia suala la deni la Italia na uwezekano wa kulipa deni hilo la taifa. Pamoja na hayo kuna athari ya moja kwa moja katika uchumi wa bara lote la Ulaya. Mzozo huo hata hivyo unaweza kutumika kama fursa kwa Italia na Umoja wa Ulaya."
Ni maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani , kama yalivyokusanywa leo na Sekione Kitojo.
Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri: Grace Patricia Kabogo