Korea Kusini yaishutumu Korea Kaskazini kwa kukiuka haki
4 Juni 2024Haya yamesemwa na balozi wa Seoul katika Umoja wa Mataifa. Hatua hiyo inatarajiwa kuighadhabisha Korea Kaskazini na huenda ikapingwa na Urusi na China.
Balozi huyo wa Korea Kaskazini joonkook Hwang anasema anatarajia kuungwa mkono pakubwa na wanachama wa Baraza la Usalama kwa kuwa suala la haki za binadamu Korea Kaskazini liko rasmi katika ajenda za baraza hilo.
Soma pia:Korea Kusini kusitisha makubaliano ya kijeshi na Pyongyang
Baraza hilo la usalama lenye wanachama 15, mara ya mwisho lilikutana Agosti mwaka jana kujadili suala hilo, katika kikao chake cha kwanza cha wazi tangu mwaka 2017.
China na Urusi wanasema kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa si taasisi inayohusika na kujadili suala hilo, bali Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Haki lililo na makao yake huko geneva, Uswisi.