1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Korea Kusini: Pyongyang bado inaturushia maputo ya taka

24 Juni 2024

Jeshi la Korea Kusini limesema Korea Kaskazini huenda ikawa imerusha maputo yenye takataka kuelekea nchini humo, hatua inayoendeleza vita vya kisasi vya kurushiana maputo baina ya mataifa hayo.

https://p.dw.com/p/4hRYA
Korea Kusini | Maputo ya taka| Korea Kaskazini
Puto lilobeba vitu kadhaa ikiwemo taka likiwa upande wa Korea Kusini huku ikiaminika limerushwa na jirani ya nchi hiyo Korea Kaskazini.Picha: Yonhap/REUTERS

Wakuu wa majeshi nchini Korea Kusini wamesema kwamba Korea Kaskazini kwa mara nyingine imerusha kile wanachodhani kuwa ni maputo yalilobeba takataka na kuongeza kuwa maputo hayo yalikuwa yakielea eneo la mpakani.

Limewaomba raia kuwa waangalifu dhidi ya takataka zinazoanguka na kutogusa chochote na badala yake wazitolee ripoti kwenye kambi au kituo cha polisi kilicho karibu.

Pyongyang tayari ilirusha maelfu ya maputo yenye takataka katika kile ilichoita kulipizia kisasi hatua ya Korea Kusini ya kurusha maputo yaliyokuwa na karatasi zilizoandikwa propaganda za kuipinga serikali ya Korea Kaskazini.