1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yazindua manowari yenye vichwa vya nyuklia

8 Septemba 2023

Korea Kaskazini imezindua manowari yake ya kwanza inayoweza kurusha mabomu ya nyuklia.

https://p.dw.com/p/4W6l8
Nordkorea l neues Atom-U-Boot "Hero Kim Kun Ok" eingeweiht
Picha: KCNA via REUTERS

Kulingana na taarifa kwenye shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya nchi hiyo, manowari hiyo itakuwa miongoni mwa nyambizi zake zinazoshika doria katika rasi ya Korea na Japan.

Akikizindia chombo hicho, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema manowari hiyo nambari 841 iliyopewa jina la Shujaa Kim Kun Ok, itakuwa moja kati ya zana zake kuu za majini.

Wachambuzi wamesema chombo hicho  kinaonekana kuwa manowari ya zama za Soviet iliyokarabatiwa ambayo Korea Kaskazini ilinunua kutoka China miaka ya 1970 na kuanza kuitengenezea nchini humo.

Korea Kaskazini imefanya majaribio kadhaa ya silaha ndani ya mwaka huu. Mwezi uliopita ilishindwa katika jaribio lake la pili la kupeleka satelaiti ya kijasusi kwenye obiti.