Korea Kaskazini yazindua manowari ya shambulio la nyuklia
8 Septemba 2023Korea Kaskazini imetangaza kuwa imeunda manowari ya kimkakati ya shambulio la nyuklia kama sehemu ya juhudi zake za kuimarisha kikosi cha wanamaji. Shirika la habari la serikali la KCNA limeripoti kwamba kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un aliongoza hafla ya uzinduzi huo na kusema kuwa manowari hiyo ni mkakati wa kujiimarisha kiusalama chini ya maji.
Manowari hiyo imepewa nambari 841 na jina la Shujaa Kim Kun Ok. Korea Kaskazini imefanya majaribio kadhaa ya silaha ndani ya mwaka huu huku mwezi uliopita ikishindwa katika jaribio lake la pili la kupeleka satelaiti ya kijasusi kwenye obiti.Korea Kaskazini: Ushirika wa Korea Kusini na Marekani utachochea uhasama
Kwa upande mwingine Korea Kusini na mshirika wake Marekani nazo pia zimeongeza ushirikiano wa kiulinzi kwa kufanya luteka za pamoja za kijeshi.