Korea Kaskazini yarusha makombora kadhaa baharini
28 Januari 2024Matangazo
Hii ikiwa ni mara ya pili kwa Pyongyang kufanya majaribio ya aina hiyo ya silaha katika kipindi chini ya wiki moja.
Kulingana na taarifa hiyo makombora hayo yalirushwa majira ya saa mbili asubuhi na kwamba mamlaka za kiitelijensia za Marekani na Korea Kusini zinafanya tathmini.
Hata hivyo haikuelezwa ni makombora mangapi yaliyorushwa na kiasi cha umbali yaliyosafiri.
Soma pia: Korea Kaskazini yafanya luteka za kijeshi mpakani na Korea Kusini
Kauli ya jeshi imesema kuwa wakati Korea ya Kusini ikiendelea kuimarisha ufuatiliaji na umakini, nchi hiyo inaendelea kushirikiana kwa karibu kijeshi na Marekani. Taarifa hiyo imeendelea kubainisha kuwa Seoul inaendelea kufuatilia ishara za zozote za ziada na shughuli za Korea ya Kaskazini.