SiasaAsia
Korea Kaskazini yafanya luteka za kijeshi katika pwani yake
7 Januari 2024Matangazo
Korea Kaskazini imefanya luteka za kijeshi katika pwani yake ya magharibi siku ya tatu mfululizo karibu na mpaka wa bahari unaozozaniwa na Korea Kusini. Jeshi la Korea Kusini limesema Korea Kaskazini imefyetua risadi zaidi ya 90 kaskazini mwa kisiwa cha Yeonpyeong hivi leo.
Jeshi hilo limeituhumu Korea Kaskazini kwa kufyetua risasi katika eneo ambalo haliruhusiwi shughuli za kijeshi lililotengwa mnamo 2018 chini ya mkataba wa kupungu hali ya wasiwasi katika rasi ya Korea, likisema ulipuajia mabomu unatishia amani ya rasi hiyo. Wakazi wa kisiwa cha mpakani mwa Korea Kusini cha Yeonpyeong walionywa wabaki ndani ya nyumba zao huku Korea Kaskazini ikifanya luteka za kijeshi karibu na mpakani.