1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kusini

Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa marefu

14 Januari 2024

Taarifa za Korea Kusini zimesema Korea Kaskazini imerusha kombora la masafa marefu lililoangukia kwenye bahari ya Japan.

https://p.dw.com/p/4bDdr
Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa marefu
Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa marefuPicha: Jung Yeon-je/AFP

Korea Kaskazini imerusha kombora la masafa marefu lililoangukia kwenye bahari ya Japan katika muktadha wa kuongezeka mivutano na matamshi ya uchochezi kutoka Korea Kaskazini.

Ingawa aina ya kombora hilo haikufahamika, nchi hiyo hivi karibuni imekuwa ikifanya majaribio ya roketi za kisasa aina ya Hwasong-18.

Bado haijabainika kombora hilo liliruka umbali gani, lakini walinzi wa pwani wa Japan wamesema kitu ambacho kinaweza kuwa kombora la masafa marefu kilichorushwa kutokea Korea Kaskazini, tayari kilikuwa kimetua.

Shirika la televisheni la Japan NHK limeripoti kuwa kombora hilo lilitua nje ya eneo la kiuchumi ,eneo la bahari ambalo linazunguka ardhi ya Japan.