1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yarusha kombora aina ya Hwasong-18

19 Desemba 2023

Korea Kaskazini imesema kuwa imerusha kombora aina ya Hwasong - 18 kama sehemu ya kuthibitisha utayari wa vita na kuonyesha uwezo wake wa silaha za nyuklia katikati ya uhasama unaoongezeka kati ya Pyongyang na Marekani.

https://p.dw.com/p/4aJxR
Nordkorea | Militärparade in Pjöngjang
Kombora la masafa marefu aina ya Hwasong-17 la Korea KaskaziniPicha: Yonhap/picture alliance

Shirika la habari la serikali KCNA limeripoti kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alihudhuria hafla ya urushaji wa kombora hilo.

Kombora hilo la Hwasong - 18 lilifika umbali wa kilomita 6,518 sawa na maili 4,050 na kulenga shabaha iliyokusudiwa.

Kim Jong Un amesema kurushwa kwa kombora hilo kunatuma "ishara wazi kwa maadui ambao wanaendeleza uhasama" dhidi ya Korea Kaskazini.

Kiongozi huyo amefafanua kuwa hio ni mojawapo ya hatua ambayo Korea Kaskazini inaweza kuchukua iwapo Marekani itafanya uamuzi mbaya dhidi yake.