1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani, Korea Kusini, Japan kukutaka kwa kujadili usalama

7 Desemba 2023

Washauri wa usalama wa mataifa ya Marekani, Korea Kusini na Japan watakutana wiki hii kujadili ongezeko la kitisho cha kijeshi kutoka Korea Kaskazini na masuala ya usalama wa kikanda.

https://p.dw.com/p/4ZtBz
USA Der neu gewählte argentinische Präsident Milei auf Besuch
Mshauri wa masuala ya usalama wa Marekani Jake SullivanPicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Mshauri wa usalama wa taifa wa Korea Kusini, Cho Tae-yong, atakuwa mwenyeji wa mkutano huo wa pande tatu utakaofanyika mjini Seoul siku ya Jumamosi. Chong, atakutana na wenzake wa Marekani Jake Sullivan na wa Japan, Takeo Akiba. Mbali na kuijadili Korea Kaskazini, mambo mengine yatakayojadiliwa ni teknolojia na biashara. Ofisi ya waziri mkuu wa Japan imesema majadiliano kuhusu Korea Kaskazini yatajumuisha uzinduzi wa kijeshi wa hivi karibuni wa satelaiti ya uchunguzi, kifaa ambacho kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amekielezea kuwa muhimu katika kufuatilia nyendo za majeshi ya Marekani na Korea Kusini, hali inayoongeza kitisho cha mashambulizi ya makombora ya nyuklia kutoka Korea kaskazini.