1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yakosoa tamko la mkutano wa kilele wa NATO

13 Julai 2024

Korea Kaskazini imekosoa vikali tamko la mkutano wa kilele wa Jumuiya ya kujihami, NATO uliomalizika mjini Washington, ambapo wamelikosoa taifa hilo kwa kuisaidia Urusi kijeshi.

https://p.dw.com/p/4iF3D
Washington | miaka 75 ya NATO
Wakuu wa mataifa wanachama wa NATO katika mkutano wa kilele wa uhirika wa kijeshi uliofanyika Washingto, MarekaniPicha: Yves Herman/REUTERS

Shirika la habari la nchini humo KNCA limearifu mapema leo, likimnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya nje aliyesema tamko la mkutano huo wa Washington, lililotolewa hadharani Julai 10 lilithibitisha kwamba Marekani na NATO vimegeuka na kuwa kama vyombo vinavyoibua kitisho kikubwa zaidi kwa amani na usalama duniani.

Alikosoa pia hatua ya Marekani ya kujitanua kijeshi na mataifa wanachama wa NATO pamoja na  washirika wa Asia akisema inaweza kuchochea pakubwa kuvuruga amani ya kikanda na usalama wa kimataifa.

Kwenye tamko lao, wakuu wa NATO walisisitizia juu ya ombi la uanachama wa Ukraine, kupinga hatua ya China kuisaidia Urusi kwenye vita vyake nchini Ukraine, na kuitaka kuacha mara moja.

Waliishutumu pia Korea Kaskazini na Iran kwa kuchochea vita hivyo, kwa kuisaidia Urusi kijeshi.