SiasaKorea Kaskazini
Korea Kaskazini yaionya Marekani
27 Aprili 2024Matangazo
Shirika la habari la serikali limemnukuu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini aliyemesema Pyongyang itafanya maamuzi magumu na thabiti ya kulinda uhuru wake na usalama katika kukabiliana na Washington inayotumia haki za binadamu kama chombo cha uvamizi dhidi ya Korea Kaskazini.
Msemaji huyo alisema hayo akiiangazia ziara ya mjumbe maalum wa haki za binadamu wa serikali ya Rais Joe Biden, Julie Turner, nchini Korea Kusini mwezi Februari na kujadili Korea Kaskazini.
Ripoti ya mwaka ya Wizara ya Mambo ya Nje imeonyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu nchini Korea Kaskazini ikiwa ni pamoja na mauaji ya kiholela, mateso na adhabu kali zinazotolewa na mamlaka.