1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yafanya majaribio ya makombora

18 Septemba 2024

Korea Kaskazini imefanya majaribio ya makombora kutokea pwani ya mashariki mapema Jumatano, siku chache baada ya kuzindua kiwanda cha kurutubisha madini ya urani na kuahidi kuboresha silaha zake za nyuklia.

https://p.dw.com/p/4kjrE
Korea Kaskaziniyajaribu makombora
Picha hii iliyopigwa Agosti 27, 2024 na kutolewa kutoka Shirika rasmi la Habari la Korea Kaskazini (KCNA) kupitia KNS mnamo Agosti 28, 2024 inaonyesha majaribio ya mfumo wa roketi wa 240mm katika eneo la siri nchini Korea Kaskazini.Picha: KCNA VIA KNS/AFP

Korea Kusini na Japan zimethibitisha taarifa hizo, wakati Wizara ya Ulinzi ya Japan iliposema Korea Kaskazini huenda imefyatua kombora la masafa marefu na walinzi wa pwani wakithibitisha kuanguka kwa kombora hilo.

Shirika la habari la Korea Kaskazini aidha, Yonhap liliripoti juu ya kufyatuliwa kwa makombora kadhaa ya masafa mafupi, likinukuu jeshi la Korea Kusini.

Haya yanafanyika siku chache baada ya taifa hilo lililotengwa kwa mara ya kwanza kuonyesha vinu vinavyozalisha mafuta kwa ajili ya mabomu ya nyuklia.