1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yafanya majaribio ya makombora ya kimkakati

23 Aprili 2024

Korea Kaskazini imefanya kwa mara ya kwanza majaribio ya silaha za kimkakati za kukabiliana na mashambulizi ya nyuklia.

https://p.dw.com/p/4f4Sp
Makombora ya Pyongyang
Kombora la masafa marefu la Korea Kaskazini chapa DPRKPicha: AFP

Shirika la habari linalodhibitiwa na serikali KCNA limeripoti kuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un alisimamia zoezi hilo.

Kulingana na taarifa ya jeshi, Pyongyang ilifyetua kuelekea baharini makombora kadhaa ya masafa marefu ambayo yalisafiri hadi kilometa 300 na kusema kuwa hiyo ni onyo kutokana na luteka ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini ambayo imelaani tukio hilo na kulitaja kuwa ni uchokozi wa ziada.

Licha ya vikwazo vya kimataifa,  Korea Kaskazini imekuwa ikiendelea kufanya majaribio ya makombora yenye uwezo wa nyuklia na mifumo mingine ya silaha katika kile wanachosema ni kukabiliana na uadui wa Marekani na jiani yake Korea Kusini.