SiasaKorea Kaskazini
Korea Kaskazini yarusha makombora ya masafa mafupi baharini
18 Machi 2024Matangazo
Korea Kaskazini imeyarusha makombora hayo wakati ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, yuko nchini Korea Kusini kuhudhuria mkutano wa tatu juu ya demokrasia.
Makao makuu ya jeshi la Korea Kusini yamethibitisha kurushwa kwa silaha hizo mapema Jumatatu.
Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida ameliambia bunge la nchi yake kwamba makombora yaliyorushwa na Korea Kaskazini yaliangukia baharini kwenye eneo lililopo kati ya Japan na rasi ya Korea.
Marekani imesema zoezi hilo linahatarisha usalama.