Korea Kaskazini haitaki mawasiliano yoyote na Japan (Kim Yo)
26 Machi 2024Yo Jong ameyasema haya siku moja tu baada ya kudai kuwa Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, alikuwa ameomba kufanya mazungumzo na kakake Kim Jong Un.
Hapo jana Kim Yo Jong ambaye ni mmoja wa wasemaji wakuu wa utawala huo, alisema haiwezekani kufanyika mkutano na Japan hadi pale Tokyo itakapobadilisha sera yake kwa Korea Kaskazini.
Lakini leo amesema hatua ya Japan kukosa ujasiri kwa ajili ya mahusiano mapya ya Korea Kaskazini na Japan, ukiwemo msimamo wake kuhusiana na suala la utekaji nyara na mipango ya kijeshi ya Korea Kaskazini.
Kihistoria mahusiano ya nchi hizo mbili yameharibika kutokana na mzozo wa muda mrefu wa utekaji nyara na mipango ya kijeshi iliyopigwa marufuku ya Korea Kaskazini.
Katika siku za hivi karibuni lakini, Waziri Mkuu Kishida ameelezea nia ya kuyaboresha, jambo ambalo Pyongyang haikulipinga.