SiasaKorea Kaskazini
Kim aongoza gwaride la kijeshi
14 Machi 2024Matangazo
Kulingana na KNCA, Kim pia alieleza kuridhishwa na namna aina mpya ya kifaru cha kivita kilivyofanikiwa kwa mara ya kwanza kuonyesha uwezo wake wa kushambulia, katika kile ambacho KNCA imekiita gwaride la mafunzo.
Shughuli hiyo ya kijeshi iliandaliwa maalumu kwa ajili ya kukagua uwezo wa kupambana wa vikosi vya vifaru na kuviwezesha kuelewa mbinu za kushambulia katika operesheni tofauti tofauti.
Mafunzo hayo ya vifaru yanachukuliwa kama jibu la siku 11 za luteka za kila mwaka za kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani zinazotarajiwa kumalizika siku ya Alhamisi. Taifa hilo linaona mazoezi ya wapinzani wake kama maandalizi ya uvamizi.