Kongo yapokea chanjo zaidi za Mpox kutoka Marekani
11 Septemba 2024Matangazo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepokea dozi 50,000 ya chanjo ya ugonjwa wa homa ya nyani kutoka Marekani baada ya kupokea chanjo nyingine 200,000zilizotolewa na Umoja wa Ulaya.
Kongo ni kitovu cha mripuko wa sasa wa maambukizi ya ugonjwa huo ikiripoti zaidi ya visa zaidi ya 21,500 na zaidi ya vifo 700, kwa mujibu wa taasisi ya afya ya umma nchini humo inayosimamia janga hilo. Chanjo kutoka Marekani ziliwasili jana Jumanne kwa mujibu wa balozi wa Marekani mjini Kinshasa, Lucy Tamlyn. Kwa ujumla kufikia sasa Kongo imepokea chanjo 265,000.