1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shehena ya kwanza ya chanjo za Mpox kuwasili Kongo Alhamisi

5 Septemba 2024

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo itapokea shehena ya kwanza ya dozi takribani 100,000 za chanjo ya Ugonjwa wa homa ya nyani, Mpox.

https://p.dw.com/p/4kIiw
DR Congo kupokea chanjo dhidi ya Mpox
Chanjo hizo za kwanza zinatoka katika kampuni ya dawa ya Bavarian Nordic ya Denmark. (Picha ya maktaba)Picha: Gideon Markowicz/Xinhua News Agency/picture alliance

Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa barani Afrika CDC, kimeseema jumla ya chanjo laki mbili zitawasili nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufikia mwishoni mwa wiki hii.

Shehena hiyo ya kwanza ya chanjo za Mpox ilitarajiwa kuwasili mjini Kinshasa majira ya saa tano asubuhi, huku shehena nyingine ya chanjo laki moja imepangiwa kuwasili kabla ya mwisho wa wiki hii.

Seŕikali ya Kongo imejiandaa kuanza zoezi la utoaji wa chanjo za Mpox mwishoni mwa juma hili.

Chanjo hizo za kwanza zinatoka katika kampuni ya dawa ya Bavarian Nordic ya Denmark.

Zaidi ya watu 17,500 wameathiriwa na mpox na wengine 629 wamekufa nchini Kongo tangu kuanza mwaka huu, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO.