1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Kitisho kikubwa kwa watu wa Gaza ikiwa UNRWA haitafadhiliwa

31 Januari 2024

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameungana kuonya juu ya athari mbaya kabisa kwa watu wa Gaza ikiwa wafadhili wakubwa wa shirika la UNRWA hayatarejesha ufadhili kwa shirika hilo muhimu kabisa kwa watu hao waliozingirwa.

https://p.dw.com/p/4btVH
Shirika la kuhudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA

Marekani na mataifa mengine yametangaza kusitisha ufadhili kwa UNRWA baada ya Israel kudai watumishi 12 wa shirika hilo walihusika na shambulizi la Oktoba 7 lililochochea vita vya Gaza.

Wakuu wa mashirika ya watoto la UNICEF, WFP, IOM na mengine pamoja na washirika wao walisema madai hayo ni ya kufedhehesha. 

Hata hivyo, wamesema kwenye taarifa yao ya pamoja kwamba si sawa kulizuia shirika hilo zima kuendelea kuwahudumia watu ambao wana mahitaji makubwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito jana Jumanne kwa mataifa 35 wafadhili katika kikao cha ndani huku akiwaomba msaada mpya.