1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kim Jong Un asifu mahusiano mazuri ya nchi yake na Urusi

13 Septemba 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amelisifu jeshi la Urusi linalopigana vita Ukraine akisema anaamini litashinda kwenye vita hivyo. Kim ameyasema hayo walipokutana na rais Vladmir Putin huko Vostochny cosmodrome.

https://p.dw.com/p/4WIns
Russland | Treffen Kim Jong Un und Wladimir Putin
Picha: Mikhail Metzel, Sputnik, Kremlin Pool Photo via AP/picture alliance

Viongozi hao wawili wamefanya mazungumzo kuhusu mahusiano ya nchi zao zilizotengwa na ulimwengu wa nchi za Magharibi. Kim Jong Un amesema mazungumzo na mwenyeji wake yaligusia masuala mbali mbali ya ushirikiano.


"Hivi punde nilikuwa na mazungumzo ya kina na Komradi Putin kuhusu hali ya kisiasa na kijeshi katika eneo la rasi ya Korea na UIaya pamoja na ushirikiano wa kimikakati,uungaji mkono na mshikamano katika mapambano ya kulinda haki ya uhuru wa mamlaka na usalama,na Kuhakikisha amani ya kudumu katika eneo hili na ulimwenguni. Tumefikia maelewano ya kuridhisha kuhusu namna ya kuimarisha kila nyanja,'' alisema Kim Jong Un.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin na kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong Un wafanya mazungumzo

Rais Putin wa Urusi kwa upande wake amesifu mustakabali wa ushirikiano imara na urafiki kati ya nchi yake na Korea Kaskazini. Aidha amewaambia waandishi habari kwamba anakiona kile alichokiita,uwezekano wa kufanyika ushirikiano wa kijeshi na Korea Kaskazini.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW