1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim Jong Un atoa wito wa maandalizi ya haraka ya vita

28 Desemba 2023

Kim amekitaka chama chake "kuongeza kasi zaidi ya maandalizi ya vita" katika sekta zote, zinazojumuisha silaha za nyuklia na ulinzi wa raia

https://p.dw.com/p/4adxe
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akihudhuria mkutano wa 5 wa kitaifa wa kina mama mjini Pyongyang mnamo Desemba 4, 2023
Kiongozi wa Korea Kaskazini - Kim Jong UnPicha: KCNA/REUTERS

Kim amesema hayo kwenye mkutano wa sherehe za mwisho wa mwaka wa chama hicho ambapo pia anatarajiwa kutangaza maamuzi muhimu ya sera kwa mwaka 2024.

Soma pia;Kim Jong Un asifu mafanikio ya Korea Kaskazini mwaka 2023

Matamshi hayo yanakuja wiki moja tu baada ya Kim kuonya kwamba nchi yake haitasita kufanya shambulio la nyuklia ikiwa "itachokozwa " kwa silaha za nyuklia.

Soma pia:Korea Kaskazini yalitaka jeshi lake liwe tayari kujibu uchokozi

Korea Kusini, Japan na Marekani zimeongeza ushirikiano wa ulinzi wakati ambapo Korea Kaskazini imefanya mfululizo wa majaribio ya silaha za nyuklia mwaka huu, na hivi karibuni zimeanzisha mfumo wa kupata data za wakati halisi kuhusu hatua za Kaskazini za kurusha makombora.