1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yalitaka jeshi kuwa tayari kujibu uchokozi

1 Desemba 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amelitaka jeshi la nchi hiyo kuwa tayari kujibu uchokozi wa aina yoyote ile utakaofanywa na maadui.

https://p.dw.com/p/4Zeca
Korea Kaskazini | Kim Jong Un
Kim Jong Un akiwa na wakuu wake wa kijeshiPicha: KCNA/KNS/AFP

Haya yamesemwa na shirika la habari la kitaifa la Korea Kaskazini KCNA, baada ya Pyong Yang kuapa kupeleka kikosi chenye nguvu zaidi cha wanajeshi na silaha mpya katika mpaka wake na Korea Kusini.

Kim ameyasema haya wakati wa ziara yake katika makao makuu ya jeshi lake la angani ambapo ametoa mwongozo wa kimkakati kwa ajili ya kuimarisha utayari wa jeshi na uwezo wake wa kushirika vita.

Soma pia: Korea Kaskazini yarejesha shughuli za kijeshi mpakani na Kusini

Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilizindua setlaiti yake ya upelelezi ambayo inasema ni ya kupeleleza nyend za kijeshi za Marekani na Korea Kusini.

Marekani na marafiki zake wamelaani vikali uzinduzi wa setlaiti hiyo wakisema ni ukiukaji wa maazimio kadhaa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.