1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim Jong Un aliamuru jeshi lake kuwa tayari kwa vita

10 Agosti 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametoa wito wa maandalizi na mazoezi zaidi ya kijeshi, ongezeko la uzalishaji wa silaha ili kujiandaa na uwezekano wa vita.

https://p.dw.com/p/4UzZT
Nordkorea Treffen der Zentralen Militärkommission der Arbeiterpartei Koreas in Pjöngjang
Kiongozo wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akifanya ukaguzi wa jeshi la nchi hiyoPicha: KCNA/REUTERS

Kim Jong Un amemfuta kazi mkuu wa jeshi la nchi hiyo Pak Su il na nafasi yake kuchukuliwa na waziri wa ulinzi Jenerali Ri Yong Gil.

Kauli ya Kim iliripotiwa na vyombo vya habari vya serikali KCNA wakati akifanya mazungumzo na tume ya Jeshi ambayo ina jukumu la kujadili mipango na hatua za kukabiliana na maadui wa Korea Kaskazini ambao hata hivyo hawakutajwa moja kwa moja.

Marekani imekuwa ikiishutumu Korea Kaskazini kuipatia Urusi silaha na makombora katika vita vyake huko Ukraine, madai yaliyokanushwa na Moscow pamoja na Pyongyang.

Marekani na Korea Kusini wanapanga kufanya luteka ya kijeshi kati ya Agosti 21 na 24, mazoezi ambayo Korea Kaskazini inayaona kama tishio kwa usalama wake.