1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Kim Jong Un aagiza makampuni kuongeza utengenezaji wa silaha

6 Agosti 2023

Kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Un ameviagiza viwanda vinavyotengeneza injini za makombora, mizinga na silaha nyingine, kuongeza uwezo wa utengenezaji wa silaha hizo.

https://p.dw.com/p/4Up3W
Kim inspiziert Munitionsfabriken in Nordkorea
Picha: picture alliance/dpa/KCNA/KNS

Kulingana na shirika la habari la Korea Kusini, Jong Un ametoa agizo hilo kama sehemu muhimu ya kukuza uwezo wa nchi hiyo kujilinda. Ametoa amri hiyo baada ya kutembelea makampuni kadhaa ya kutengeneza silaha aliyoifanya Alhamisi hadi Jumamosi.

Soma pia:Kim Jong Un akutana na wajumbe kutoka Urusi na China

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini amefanya ziara hiyo wakati Pyongyang ikipambana kutengeneza silaha za kimkakati na za kawaida huku ikifanya maonesho makubwa ya silaha zake.

Hayo yanaendelea wakati ambapo Marekani mara kadhaa imekuwa ikituhumu Korea ya Kaskazini kwa kuipatia Urusi silaha kwa ajili ya vita dhidi ya Ukraine. Silaha hizo ni pamoja na roketi na makombora yanayodaiwa kupelekwa kwa mamluki wa Wagner. Urusi na Korea zimekanusha tuhuma hizo.