1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Helene chakaribia kwa kasi huko Florida

27 Septemba 2024

Kimbunga Helene kimevuka Ghuba ya Mexico kuelekea Florida, na hivyo kuzusha hali ya hofu katika sehemu za kaskazini-magharibi mwa jimbo La Florida, Marekani.

https://p.dw.com/p/4l98P
Kimbunga Helene mjini Florida
Kimbunga Helene mjini FloridaPicha: Joe Raedle/Getty Images

Kimbunga Helene kimevuka Ghuba ya Mexico kuelekea Florida, na hivyo kuzusha hali ya hofu katika sehemu za kaskazini-magharibi mwa jimbo La Florida, Marekani.

Mvua kubwa, mafuriko na upepo mkali unaokadiriwa kuwa na kasi ya zaidi ya kilometa 150 kwa saa vinatarajiwa kushuhudiwa katika sehemu kubwa ya kusini mashariki mwa jimbo hilo.

Hali ya dharura imetangazwa katika majimbo ya Florida, Georgia, Carolina, Virginia na Alabama. Maelfu ya watu wamehamishwa huku kaya zaidi ya 340,000 zikiwa hazina umeme huko Florida.