JangaMarekani
Maelfu ya watu wahamishwa Florida wakihofia kimbunga Helene
26 Septemba 2024Matangazo
Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga leo Alhamisi, na kulingana na mamlaka kinaweza kuwa janga na kusababisha vifo.
Kituo cha utabiri wa matukio ya vimbunga nchini Marekani (NHC) kimesema kimbunga hicho kinatarajiwa kusababisha upepo mkali, mawimbi na mvua kubwa katika sehemu pana ya jimbo hilo. Gavana wa Florida Ron DeSantis ametangaza hali ya dharura kwa karibu kaunti zote 67 katika jimbo hilo.
Upepo kwa sasa umekadiriwa kufikia kasi ya kilomita 140 kwa saa na kimbunga hicho kinaweza kuipiga Florida leo jioni baada ya kupiga eneo la kitalii la Yucatán huko Mexico. Majimbo kadhaa yaliyo jirani na Florida yako katika hali ya tahadhari ikiwa ni pamoja na jiji la Atlanta lenye wakazi milioni tano.