1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim Jong Un athibitisha tena kuimarisha uhusiano na Putin

16 Agosti 2024

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amethibitisha tena ahadi yake ya kuimarisha ushirikiano na Urusi katika wa ujumbe kwa Rais Vladimir Putin.

https://p.dw.com/p/4jWsu
Korea Kaskazini - Mzozo wa Korea - Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amerudia tena kuahidi kuimarisha uhusiano na Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: /kcna/kns/dpa/picture alliance

Kim ametoa ujumbe huo kwenye maadhimisho ya uhuru wa Pyongyang kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Japan.

Shirika la habari la serikali KCNA limesema leo kwamba Kim alikuwa akijibu ujumbe wa pongezi kutoka kwa Putin kwenye kumbukumbu hizo, ambaye aliusifu ushirikiano ulioanza tangu wanajeshi wa Soviet walipoisaidia Korea Kaskazini kupambana na Japan, ambao umeendelea kuwa msingi wa uhusiano wao.

Kim na Putin walifanya mkutano wa pili wa kilele mwezi Juni mjini Pyongyang na kusaini makubaliano mapana ya ushirikiano wa kimkakati uliojumuisha mkataba wa ulinzi.