1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man United yakaribia kuaga Champions, Munich ikifuzu 16

9 Novemba 2023

Manchester United ya England inakaribia kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufungwa mabao 4-3 na FC Copenhagen.

https://p.dw.com/p/4Yahe
Kikosi cha Bayern Munich kimefanikiwa kutinga hatua ya 16 ya michuano ya Champions barani Ulaya baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Galatasaray
Kikosi cha Bayern Munich kimefanikiwa kutinga hatua ya 16 ya michuano ya Champions barani Ulaya baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya GalatasarayPicha: Bernd Feil/M.i.S./IMAGO

Marcus Rashford alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumkanyaga  Elias Jelert, hali iliyokiyumbisha zaidi kikosi hicho ambacho tayari kimefungwa mara tatu katika michezo minne na hivi sasa kikishika mkia kwenye kundi A.

Kocha wa United Erik Ten Hag amesema matokeo hayo ni ya kusikitisha wakati sasa wakiwa na pointi 3, ingawa ameukosoa uamuzi aliosema ulikuwa ni mkali wa mwamuzi wa mchezo ambaye amesema ni kama hakuwa na uhakika. 

United imebakiwa na michezo miwili, kati yake na Galatasaray na Bayern Munich ya Ujerumani.

Real Madrid, mabingwa mara 14 wa Champions tayari wametinga 16 bora baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Braga ya Porto, huku pia ikiwa imebakiwa na michezo miwili mkononi.

Harry Kane alifanikiwa kuisaidia Bayern Munich ya Ujerumani pia kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuifungia mabao 2-1 dhidi ya Galatasaray. Bayern pia ina michezo miwili kibindoni.