Khamenei: Adhabu kali kwa Israel baada ya mauaji ya Haniyah
31 Julai 2024Katika taarifa iliyorushwa na shirika la habari la IRNA, Khamenei amesema kwa hatua hiyo, nikinukuu, ''mhalifu na utawala wa kigaidi wa Kizayuni'', umejitayarishia msingi wa adhabu kali.
Khamenei ameongeza kuwa wanaona ni jukumu lao kulipiza kisasi kwasababu Haniyeh ameuawa katika ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
"Tunazingatia sana tukio hili. Tunapinga na kulaani vikali kitendo cha mauaji. Tuna wasiwasi mkubwa kwamba tukio hili linaweza kusababisha kuongezeka kwa machafuko katika eneo hili. China daima imekuwa ikitetea utatuzi wa migogoro ya kikanda kwa njia ya mazungumzo," ilisema China kupitia msemaji wake wa wizara ya mambo ya nje Lin Jian.
Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh auwawa Iran
Kundi la Hamas limedai kuwa Haniyeh aliuawa kwenye makazi yake mjini Tehran katika shambulio la anga la Israel baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa kiongozi mpya wa Iran.
Hata hivyo Israel haijatoa tamko kuhusu tukio hilo.