1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yathibitisha kisa cha kwanza cha corona

Josephat Charo
13 Machi 2020

Kisa cha kwanza cha virusi vya corona kimeripotiwa nchini Kenya. Wizara ya Afya nchini humo imesema kuwa kisa hicho kilithibitishwa Alhamisi (12.03.2020) Mkenya huyo alisafiri kutoka Marekani tarehe tano Machi.

https://p.dw.com/p/3ZLMe
Coronavirus in USA Kirkland Reinigungsteam in Schutzkleidung
Picha: AFP/Getty Images/J. Moore

Kenya imetangaza kisa cha kwanza cha virusi vya corona Ijumaa. Mwanamke raia wa nchi hiyo ambaye alirejea nyumbani akitokea nchini Marekani, alipatikana na maambukizi baada ya kupimwa mjini Nairobi. 

Waziri wa afya wa Kenya, Mutahi Kagwe, amethibitisha kisa hicho akisema mama huyo alipitia mjini London, Uingereza alipokuwa akirejea nyumbani mnamo tarehe 5 mwezi Machi. 

Hiki ni kisa cha kwanza cha virusi vipya vya corona katika eneo la Afrika Mashariki.