1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaKenya

Kenya yasema rushwa ndio imechangia mlipuko wa gesi

Sylvia Mwehozi
2 Februari 2024

Msemaji wa serikali ya Kenya Isaac Mwaura amesema rushwa na ukosefu wa ufuatiliaji katika taratibu za vituo vya gesi, ndivyo vimechangia mlipuko mkubwa wa lori la mitungi ya gesi.

https://p.dw.com/p/4byx6
Timu ya wazima moto wakikabiliana na moto katika eneo la Embakasi mjini Nairobi
Timu ya wazima moto wakikabiliana na moto katika eneo la Embakasi mjini NairobiPicha: Luis Tato/AFP

Mlipuko huo ulisababisha vifo vya watu watatu usiku wa kuamkia leo na kuwajeruhi takribani watu wengine  300 mjini Nairobi.

Mlipuko huo umeteketeza ghala la nguo lililokuwa karibu na kuharibu magari kadhaa na mali za wafanyabiashara na makazi.

Akizungumza kutokea eneo la mkasa, msemaji wa serikali Isaac Mwaura amesema kituo hicho cha kujaza gesi kilikuwa kinyume cha sheria.

Mamlaka inayodhibiti nishati Kenya EPRA pia imesema ilikataa mara tatu maombi ya kampuni hiyo kupewa kibali cha kuweka kituo chake cha kuhifadhi na kujaza gesi katika eneo hilo ambapo mlipuko ulitokea kwa sababu, ni sehemu yenye wakaazi wengi.