1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yachunguza kifo cha wakili aliyetuhumiwa kwa hongo

27 Septemba 2022

Polisi nchini Kenya wanachunguza kifo cha mwanasheria aliyetuhumiwa kuwahonga na kuwatishia mashahidi katika kesi iliyotupiliwa mbali na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu - ICC dhidi ya Rais William Ruto.

https://p.dw.com/p/4HOUf
Niederlande | Internationaler Strafgerichtshof in Den Haag
Picha: Peter Dejong/AP/picture alliance

Paul Gicheru alikuwa ametuhumiwa na waendesha mashitaka wa ICC kwa kile walisema ni mpango mbaya na wenyewe madhara wa kuwaathiri mashahidi ambao ulifanya iwe vigumu kuyachunguza madai dhidi ya Ruto kuhusiana na machafuko ya baada ya uchaguzi ya mwaka wa 2007 na 2008 nchini Kenya.

Kesi yake ilifunguliwa Februari mwaka huu na Gicheru alikuwa amekanusha madai hayo. Afisa mmoja mwandamizi wa polisi ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema taarifa walizo nazo kutoka kwa familia yake ni kuwa alipata chakula na kwenda kulala na hakuamka tena. Alipatikana akiwa amefariki nyumbani kwake jana usiku.

Afisa huyo amesema mwanawe wa kiume alipelekwa hospitali kutokana na matatizo ya tumbo baada ya kula chakula hicho pamoja na baba yake.

Madai dhidi yake yalifunguliwa Februari mwaka huu akidaiwa kuwahonga mashahidi hao hadi shilingi milioni moja za Kenya.