Kenya: Mashambulizi yachangia mpaka na Somalia kutofunguliwa
5 Julai 2023Kenya imesema kuwa inachelewesha mpango wa kufungua tena mpaka wake na Somalia baada ya mashambulio kadhaa mabaya kwenye ardhi yake yanayodaiwa kufanywa na kundi la wanamgambo la Al-Shabaab.
Waziri wa mambo ya ndani Kithure Kindiki amesema ufunguaji huio wa awamu wa vivuko katika kaunti za Mandera, Lamu na Garissa kwenye mpaka mregu na Somalia, hautafanyika kama ilivyokuwa imetangazwa mwezi Mei.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya mauaji ya raia watano na vifo vya askari polisi wanane katika matukio tofauti karibu na mpaka mwezi uliopita, yaliolaumiwa kwa Al-Ashabaab. Mpaka huo ulifungwa rasmi Oktoba 2011, kutokana na mashambulizi ya Al-Shabaab, ambalo limekuwa likiendesha uasi dhidi serikali kuu mjini Mogadishu kwa zaidi ya miaka 15 sasa.
Kivuko cha Mandera kilipaswa kufunguliwa katika muda wa siku 30 tangu kutolewa tangazo hilo, kikifuatia na Garissa katika siku 60 na Lamu ndani ya siku 90.