Rais wa Kenya William Ruto amefanya mazungumzo na mwenzake wa Marekani Joe Biden mjini Washington usiku wa kuamkia leo na kila upande ukatoa ahadi ya kuendeleza mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi baina ya nchi hizo mbili. Mbali na masuala ya ulinzi, Marekani ni mshirika muhimu wa kiuchumi kwa Kenya. Sikiliza mahojiano kati ya Rashid Chilumba na mchumi Frederick Mweni akiwa mjini Nairobi.