1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya imeivunja bodi ya soka kwa tuhuma za rushwa

12 Novemba 2021

Shirikisho la kandanda duniani – FIFA limetishia kuipiga Kenya marufuku kama uamuzi wa Wizara ya michezo wa kuiteuwa kamati ya muda ili kusimamia shughuli za Shirikisho la Kandanda nchini humo – FKF hautabatilishwa.

https://p.dw.com/p/42usY
Schweiz FIFA Schriftzug Hauptquartier in Zürich
Picha: Reuters/R. Sprich

Onyo hilo la FIFA limetolewa saa chache tu baada ya Waziri wa Michezo Amina Mohammed kuwatimua maafisa wa FKF wakiongozwa na mwenyekiti wao Nick Mwendwa kufuatia madai ya rushwa.

FIFA hata hivyo imejitolea kuwa mpatanishi kati ya Wizara ya Michezo, na viongozi wa sasa wa FKF ili kupata suluhisho kwa mkwamo uliopo ambao ulisababisha Waziri Amina kuunda kamati ya mpito ya wanachama 12 itakayosimamia kandanda kwa kipindi cha miezi sita.

Wizara ya Michezo iliivunja FKF kutokana na mapendekezo ya ripoti ya uchunguzi kuhusu matumizi ya fedha ya shirikishohilo. Amina amesema uchunguzi huo ulioendeshwa kwa siku 16, ulizingatia sheria na kanuni zote.

Kiini cha uamuzi wa kuvunjwa uongozi wa Shirikisho la Kandanda la Kenya FKF

Kenia Amina Mohamed als Finanzministerin nominiert
Waziri wa Michezo wa Kenya, Amina MohamedPicha: Getty Images

Hata hivyo maadai ya matumizi mabaya ya fedha katika shirikisho hilo yalianza kuibuliwa mwaka 2017 chini ya rais wa shirikisho hilo Nick Mwendwa. "Kufuatia mapendekezo hayo na kuhifadhi heshima ya michezo na hasa kandanda, nimeamua kuteua kamati ya muda ya kusimamia kandanda, itakayokuwepo kwa kipindi cha miezi sita.”

Katika barua iliyotumwa kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa FKF Barry Otieno, FIFA imeiambiaFKF kumuarifu waziri kuwa kama hatoubatilisha uamuzi wake wa kuunda kamati ya muda, basi hawatakuwa na budi ila kuwasilisha suala hilo kwa ofisi ya Baraza Kuu kwa ajili ya kuzingatiwa na kuchukuliwa maamuzi.

Kamati ya uchunguzi ilisema kuwa maafisa wa FKF, walizembea kutoa maeleo muhimu kuhusu matumizi ya fedha. Mwanahabri wa kujitegema Milton Nyakundi ndiye chanzo cha kuvunjwa kwa FKF. Alianza kufichua maovu kwenye shirikisho hilo mwaka 2017.

Uamuzi wa serikali umekuwa ukisubiriwa na Wakenya wengi, kwani timu ya mpira ya Harambee Stars haijakuwa ikifanya vyema kutokana na kile wanachokitaja kuwa uongozi mbaya. Aidha wachezaji wa vilabu vya mpira wamekuwa wakilalamikia uongozi mbaya wa FKF.

Chanzo: DW, Nairobi